Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

George Job: Kiwango cha Djuma Shaban kimeporomoka

Djuma Shaban Kisasi.jpeg Djuma Shaban

Mon, 1 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kupitia #SportsArena ya #WasafiFm mchambuzi George Job amesema kuwa katika msimu huu wa 2022/23 kiwango cha beki wa kulia wa Yanga, Djuma Shaban kimeshuka tofauti na msimu uliopita.

“Ukiachana na Injury, performance ya Djuma imekuwa too flat msimu huu, hajawa yule wa msimu uliopita, msimu uliopita ulikuwa ukizungumzia right back ulikuwa unamtaja Djuma Shaban over hata Kapombe.

“Lakini kwa msimu huu unaweka question mark nyingi sana, kwenye mechi nyingi performance yake imekuwa flat sana nadhani anahitaji kuongeza juhudi.

“Kuna wakati alikuwa anazungumziwa uzito akapungua lakini bado hajarudi kwenye kiwango au ubora wake ambao watu wengi walikuwa wanauzungumzia,” amesema George Job.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: