Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi ni zaidi ya Nabi na Robertinho?

Gamondi X Robertinho Tanga Miguel Gamondi na Robertinho

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taratibu Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi ameanza kuwa kwenye viatu vya Nasreddine Nabi kutokana na mbinu zake kufanana na za Nabi aliyewahi kuwa kocha kikosini hapo.

Nabi alikuwa imara kwenye mbinu za kubadili mchezo kwa kutumia wachezaji walioanza kusugua benchi na walipoingia waliwapa tabasamu mashabiki na wachezaji kiujumla.

Ikumbukwe kwamba katika mchezo wa kimataifa zama za Nabi kwenye mchezo dhidi ya Club Africain ugenini ni Aziz Ki alipachika bao hilo kwenye mchezo uliochezwa Novemba 9, 2022 wakiwa ugenini.

Aziz Ki alipachika bao hilo akitokea benchi ilikuwa zama za Nabi na ilikata tiketi ya kutinga hatua ya makundi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika. Safari ilikwenda mpaka fainali ya michuano hiyo.

Chini ya Gamondi, ngoma imeanza taratibu kujibu ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya ASAS Djibout uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Agosti 26.

Katika mchezo huo mastaa wawili wa Yanga waliingia wakitoekea benchi ikiwa ni Clement Mzize na Pacoume Zouzoua hawa wawili walifunga bao mojamoja kwenye mchezo huo.

Mwisho ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Yanga 5-1 ASAS Djibout na Yanga inasonga mbele katika hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika inatarajiwa kumenyana na Al Merrikh ya Sudan.

Katika upande wa kutandaza soka la burudani Gamondi ameonekana kumfunika Kocha wa Simba Mbrazil Roberto Oliviera "Robertinho" kwani Yanga wanaonekana kucheza soka la kuvutia licha ya kutokaa pamoja kwa muda mrefu.

Mara kadhaa Mashabiki wa Simba wamesikika hadharani wakimsifu Gamondi kwa soka safi wanalocheza Yang.

Je Gamondi anwazidi uwezo Nabi na Robertinho kwa kipindi hiki kifupi alichojiunga na Yanga? Tupe maoni yako

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: