Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi awapeleka Yanga 'beach'

Yanga Gamondi As Kocha Gamondi

Sun, 3 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi raia wa Argentina, ameamua kuwapeleka ufukweni wachezaji wote wa kikosi hicho ikiwa ni maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Merrikh ya Sudan.

Yanga ambayo imeanza msimu huu kwa mafanikio kutokana na kutoa vipigo vizito katika Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika, Septemba 16, mwaka huu inatarajiwa kuwa ugenini kupambana na Al Merrikh ukiwa ni mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya kwanza.

Baada ya mchezo huo ambao umepangwa kupigwa nchini Rwanda, timu hizo zinatarajiwa kurudiana Dar, Septemba 30, mwaka huu. Mshindi wa jumla atafuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo, huku atakayepoteza, safari itaishia hapo kwa msimu huu.

Kocha huyo ambaye anaonekana amepania kuweka rekodi ya Yanga kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, juzi aliwapeleka wachezaji wa timu hiyo gym katika viwanja vya Gymkhana, huku akipanga kesho Jumatatu kuwapeleka Ufukwe wa Coco kwa ajili ya kujenga stamina zaidi.

Gamondi amechukua hatua hiyo ikiwa Ligi Kuu Bara imesimama kwa takribani wiki mbili kupisha ratiba ya mechi za timu za taifa kufuzu AFCON.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: