Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi awaita Mashabiki wa Yanga kwa Mkapa

Gamondi Awaita Mashabiki Miguel Ángel Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga

Fri, 21 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa kesho ndio Julai 22, Kilele cha Wiki ya Mwananchi, Kocha Mkuu wa Yanga katika Mkutano na waandishi wa Habari ameainisha namna anavyokiandaa kikosi chake kuelekea mchezo wa kirafiki dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika ya Kusini.

Akizungumza Gamondi amewataka Mashabiki kuja kwa wingi kuisapoti Timu yao huku akitanabaisha kuwa mchezo huo ni miongoni mwa maandalizi ya kuijenga timu kuelekea msimu mpya 2023/24.

"Kesho ni siku kubwa kwa Mashabiki wa Young Africans SC pamoja na sisi wote tunakwenda kupata nafasi ya kusherekea kufunguliwa kwa msimu huu mpya tukiwa na matarajio ya kuendelea kuipambania Klabu hii kubwa yenye historia kubwa"

"Kwenye upande wa timu bado tuko kwenye maandalizi, na mchezo wa kesho dhidi ya Kaizer Chiefs tutautumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi yetu kwa msimu ujao"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: