Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi aanza kambi kimkakati

Yanga Gift Kibabage Gamondi aanza kambi kimkakati

Sat, 15 Jul 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kule kambi ya Yanga AVIC Town kuna kazi ya kiume imeanza ambapo kocha mpya wa timu hiyo, Miguel Gamondi na jamaa kama wachezaji wa kikosi chake watashika anachotaka kifanyike kuna soka kubwa litapigwa msimu ujao.

Baada ya ratiba ya juzi wakipiga mazoezi mara mbili kwa siku wakianzia gym, kisha uwanjani jioni na jana timu hiyo iliingia katika siku ya pili kwa ratiba ngumu ya kuingiza pumzi ya kushiba wakianza kuimarisha vifua kwa soka wanalotaka kwa kuanzia gym kisha kwenda uwanjani tena.

Gamondi mapema katika kikao na mastaa wake amewaambia wachezaji wake anataka kila mchezaji ajipange kucheza soka la malengo kwa kucheza soka la chini akilenga kuona wanacheza pasi za chini.

Mbali na mpira kuwekwa chini kocha huyo ametaka soka la malengo pia lipigwe na kikosi chake akitaka timu ifike kwa kasi lango la wapinzani kisha kufungwe mabao.

Kocha huyo amekuwa mkali akiona mchezaji anamalizia nafasi kwa uzembe kwa kukosa bao hatua ambayo iliwafanya mastaa wake kujikuta wako kwenye presha wanapokaribia langoni kwa kufunga.

Muda mrefu Gamondi amekuwa akiwasisitiza wachezaji wake kucheza soka la pasi za kutosha wakielekea golini kwa wapinzani na sio zile za kurudi nyuma akiwa mkali mchezaji wake anapopiga pasi za pembeni au kurudi nyuma.

Taarifa kutoka kwa mabosi wa Yanga ni kwamba tayari kocha hiyo amesharidhika na mastaa wengi wa timu hiyo juu ya viwango vyao, huku akitaka kujipa nafasi ya kuwasoma zaidi baadhi yao ambao bado hajaona ubora wao mkubwa.

Mwanaspoti linafahamu kuwa kocha huyo atafanya maamuzi yake kwa baadhi ya mastaa wa kikosi hicho ndani ya wiki moja kutoka jana atakapowasoma zaidi katika mazoezi hayo ya wiki ya kwanza, huku tayari akiwa na majina ya nyota ambao awatafyeka.

Miongoni mwa wanaotajwa kuwa kwenye hatari zaidi ya kufyekwa ni wenye umri mkubwa kikosini sambamba na kushindwa kumuonyesha mambo mazoezini, lakini jina la Djuma Shaban na Zawadi Mauya yakitajwa sana na hasa baada ya kuingia kwa Jonas Mkude na kuwa na mzungumzo na beki wa kulia kutoka Asec Mimosas, Kouassi Attohoula Yao

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: