Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi aahidi kufuata nyayo za Kocha Nabi Yanga

Nabi Gamondi 2 WA0002 Gamondi aahidi kufuata nyayo za Nabi Yanga

Sat, 22 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu Yanga SC Miguel Gamondi amesema amekuja nchini Tanzania kuendeleza yale mazuri ambayo yaliachwa na kocha Nasserdi Nabi hivyo wanachama na wapenzi wa klabu hiyo watarajie kuona mpira mzuri na kila mchezaji akipata nafasi ya kucheza ndani ya kikosi chake.

Akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa ya Julai 21, 2023 ,Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar Es Salaam Kocha Gamandi amesema kuwa ana cv kubwa katika ufundishaji wa soka la Afrika na pia hadi muda bado sijapata kikosi cha kwanza.

“Nataka kila mchezaji ajipange kucheza soka la Malengo kwa kucheza soka la chini kwa kulenga kuona wakicheza pasi za chini,“ amesema Miguel Gamondi kocha Mkuu Yanga SC.

“Kesho (leo) ni siku kubwa kwa Mashabiki wa Young Africans SC pamoja na sisi wote tunakwenda kupata nafasi ya kusherekea kufunguliwa kwa msimu huu mpya tukiwa na matarajio ya kuendelea kuipambania Klabu hii kubwa yenye historia kubwa.

“Kwenye upande wa timu bado tuko kwenye maandalizi, na mchezo wa kesho dhidi ya Kaizer Chiefs  tutautumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi yetu kwa msimu ujao.

“Tunatarajia kuwa na malengo makubwa zaidi kwa sababu hii ni Klabu kubwa yenye mashabiki wengi wenye nguvu na ushawishi kutaka Klabu hii iendelee kufanya vizuri zaidi hasa kwenye mashindano ya kimataifa," amesema Gamondi.

Kikosi cha Yanga SC kinataraji kushuka dimbani Jumamosi Julai 22, 2023 kinataraji kucheza mchezo wa kirafiki wakimataifa dhidi ya Kaizer Chief ya Afrika kusini uwanja wa Benjamin Mkapa majira ya saa moja usiku kwenye kilele cha siku ya Mwananchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: