Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi aachiwa msala wa Kaze Yanga

Nabi X Kaze Ahadi Gamondi aachiwa msala wa Kaze Yanga

Wed, 5 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Msaidizi wa Yanga Mrundi, Cedric Kaze huenda asiwe katika sehemu ya benchi la ufundi la timu hiyo, kutokana na kushindwa kufikia muafaka na mabosi wake katika mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya.

Kaze ni sehemu ya viongozi wa benchi la ufundi la timu hiyo, ambalo limeipa mafanikio makubwa Yanga katika msimu uliopita huku wakimaliza mikataba yao ya kuendelea kubakia hapo.

Tayari aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mtunisia Nasreddine Nabi ameondoka hapo huku akitajwa kujiunga na klabu ya FAR Rabat ya nchini Morocco.

Taarifaa ambazo imezipata Championi Jumamosi, Kaze ameshindwa kufikia muafaka mzuri wa kuongeza mkataba mpya wa kubakia hapo kutokana na Yanga kushindwa kufika katika mshahara ambao anataka alipwe.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, uongozi umeweka mshahara mdogo ambao yeye ameukataa huku akiomba aboreshewe zaidi ya ule ambao aliokuwa akilipwa awali ni siri.

Aliongeza kuwa rasmi mazungumzo yamefungwa kwa pande zote hizo mbili, na hivi sasa ameachiwa Kocha Mkuu mpya wa timu hiyo, Muargentina, Miguel Gamondi kutafuta kocha msaidizi atakayekuja kufanya naye kazi.

“Uongozi wa Yanga wamemtega Gamondi wakimuachia nafasi ya kutafuta wasaidizi wake watatu katika benchi lake la ufundi wakiwemo kocha wa mazoezi ya viungo, kocha wa makipa na mtaalamu wa kuchambua mikanda ya wapinzani.

“Nafasi hizo ziliachwa wazi kufuatia kuondoka kwa Milton Nienov ambaye alikuwa kocha wa makipa, Helmy Gueldich aliyekuwa kocha wa mazoezi ya viungo na Khalil Ben Youssef na Kaze ambao wote mikataba yao imemalizika.

“Yalikuwepo mazungumzo yanaendelea kati ya Kaze na uongozi wa Yanga ambayo yameshindwa kufikia muafaka mzuri baada ya yeye kutaka aboreshewe mshahara wake, upo uwezekano mkubwa wa kocha huyo kutoendelea hapo,” alisema mtoa taarifa huyo.

Meneja wa Habari wa timu hiyo, Ally Kamwe hivi karibuni alizungumzia hilo kwa kusema kuwa: “Suala la Kaze lipo chini ya kocha wetu mpya Gamondi ambaye yeye ndiye atakayeamua, kwani kama akipendekeza alete benchi jipya basi tutaangalia nafasi nyingine tutakayompa katika timu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: