Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Nakuja kuwapa furaha Wananchi

Miguel Angel Gamondi.jpeg Kocha Gamondi

Sat, 24 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu mpya wa Klabu ya Yanga, Miguel Angel Gamondi amesema kuwa anafuraha kubwa kujiunga na Yanga kwani ni miongoni mwa klabu kubwa na yenye historia nzuri ya kisoka barani Afrika.

Kupitia video yake iliyopostiwa kwenye kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya Yanga, Gamondi ambaye ametangazwa leo na uongozi wa Yanga kuchukua nafasi ya Nassredine Nabi amesema yupo tayari kuwapa furaha Wananchi.

"Habari Wananchi! Naitwa Gamondi kutoka Argentina, kocha wa soka ambaye nina uzoefu wa zaidi ya miaka 20 kwenye soka la Afrika. Nimefundisha vilabu kama Wydad Casablanca, Mamelodi Sundowns, Belouizdad na Esperance De Tunis na nimepata mafanikio makubwa nikiwa na vilabu hivyo kwa nyakati tofauti.

"Nina furaha kubwa kujiunga na Yanga, ni miongoni mwa timu kubwa barani Afrika na ina historia kubwa kwenye Bara la Afrika kwangu mimi ni moja ya klabu kubwa kwenye bara hili, yenye heshima kubwa na mashabiki wengi na wenye hamasa.

"Ninaamini kama tutafanya kazi pamoja na viongozi, wachezaji, benchi la ufundi na mashabiki ninaamini tutaendelea kupata matokeo mazuri na mafanikio makubwa zaidi. Tutaonana siku za hivi karibuni, Daima mbele, nyuma mwiko!," amesema Gamondi.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: