Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Mabadiliko yametuokoa

Gamondi Awaita Mashabiki Miguel Gamondia.

Thu, 10 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondia amesema kuwa walistahili kupata ushindi dhidi ya Azam FC kutokana na kikosi chake kuwa bora kwenye kila eneo.

Gamondi amesema hayo mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii uliopigwa katika Dimba la Mkwakwani Tanga na Yanga kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-0.

Yanga imetumia dakika 5 tu kuamua mchezo huo kwa mabao ya kiungo mshambuliaji, Mburkinabe Stephane Aziz Ki dakika ya 85 na Clement John Mzize dakika ya 89.

“Nilitegemea mechi itakuwa ngumu, uwanja haukuwa rafiki sana kwetu kucheza mpira, kipindi cha kwanza kilikuwa kigumu, tukumbuke huu ulikuwa ni mchezo rasmi wa kwanza kwa hiyo hata wachezaji wamekaa nje bila kucheza kwa muda.

“Lakini kipindi cha pili tulikuwa superb, tuliutawala mchezo na hawakutenegeneza nafasi hata moja, tumetengeneza nafasi zaidi ya sita hatukuzitumia lakini mabadiliko yetu yalikwenda kutusaidia kupata mabao nah ii inaonyesha ubora wa hali ya juu tulio nao.

“Nina furaha kubwa na ninawapongeza wachezaji wangu na kongole ziende kwa mashabiki wa Yanga pia, kwa sababu ni wao wanatufanya tupambane. Lengo letu ni kuendelea kuboresha kikosi, kucheza mmoja mmoja na kuwa bora kwenye kila eneo siku kwa siku,” amesema Gamondi.

Yanga sasa inasubiri mshindi wa mchezo wa leo kati ya Singoida Fountain Gate na Simba, ambaye atashinda watakutana kwenye fainali huku Azam akisubiri atakayeshindwa mchezo wa leo atakutana naye kwenye mchezo wa mshindi wa tatu.

MECHI 6 ZA MWISHO Yanga v. Azam

• Yanga SC 2:0 Azam FC

• Yanga SC 1:0 Azam FC

• Azam FC 2:3 Yanga SC

• Yanga SC 2:2 Azam FC

• Azam FC 1:2 Yanga SC

• Yanga SC 2:0 Azam FC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: