Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Hili ndilo soka ninalotaka Yanga

Miguel Gamondi Xx Dickson Job Gamondi: Hili ndilo soka ninalotaka Yanga

Thu, 24 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa soka walilocheza jana dhidi ya KMC ndio aina ya mpira ambao anataka kuuona kikosi chake kinacheza msimu mzima.

Gamondi amesema hayo jana mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo ambao ulikuwa wa kwanza kwake kwenye Ligi Kuu ya Tanzania na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 5-0.

Yanga walikuwa haraka kukaba, kupora mipira, kumiliki soka, kupiga pasi za haraka, kushambulia kwa kasi kubwa na soka la burudani hali iliyowafanya KMC kuutafuta mpira muda mwingi badala ya kutengeneza nafasi.

"Tumepeta alama tatu na kujiamini kwa timu, tumeonyesha tupo kwenye njia sahihi. Nadhani tumecheza soka safi, wachezaji wametoa kila walicho nacho. Kumbukeni tumecheza na timu nzuri sana.

"Tulikuwa tumejipanga vizuri, tulikuwa makini na fit, ninawapongeza sana wachezaji wetu na nina furaha kwa sababu tumewapa mashabiki wetu kile walichostahili kukipata nah ii ndiyo soka ambayo tunataka kuicheza.

"Leo (jana) tunasherekea lakini kesho (leo) tunapaswa kuanza kujiandaa na mechi ijayo ya Kombe la Mabingwa Afrika dhidi ya ASAS FC, Jumamosi ijayo.

"Tutacheza kwa ajili ya kuwa mabingwa huwezi kusema unauona ubingwa kwenye mechi moja wakati bado kuna mechi 29, tunahitaji kuziheshimu timu zote, nadhani timu nyingi zinataka kufanya vizuri, wanahitaji kuifunga Yanga, kwa hiyo sahau kuhusu ubingwa wa Yanga wa mwaka jana huu ni msimu mpya.

"Ni safari ndefu kucheza lakini cha muhimu ni kucheza kwa kujiamini na kuhakikisha tunapata alama tatu kwenye kila mchezo wetu ili kuwapa furaha mashabiki zetu," amesema Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: