Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

GSM atoa kauli ya kibabe Yanga akielekea Congo

Gsm Gtr.jpeg GSM atoa kauli ya kibabe Yanga akielekea Congo

Fri, 31 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bosi wa Yanga, Ghalib Said Mohammed ‘GSM’ jana Alhamisi kwa mara ya kwanza alisafiri na kikosi cha timu kwenye safari ya mashindano rasmi na kutoa tamko zito kuwa Yanga wanautaka ubingwa wa mashindano hayo.

Yanga ndio wawakilishi pekee wa Tanzania katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo kwenye mashindano hayo mpaka sasa wanaongoza msimamo wa kundi D baada ya kufanikiwa kukusanya pointi 10 katika michezo yao mitano ya kwanza.

GSM pamoja na baadhi ya viongozi wa juu wa Yanga akiwemo rais wao Injinia Hersi Said na Makamu wa Rais, Arafati Haj jana Alhamisi waliongozana na sehemu ya kikosi cha wachezaji wa Yanga ambao hawakuwa na majukumu ya timu za Taifa kuelekea nchini DR Congo kwa ajili ya mchezo wao wa mwisho wa kukamilisha ratiba ya hatua ya makundi watakapovaana na TP Mazembe, utakaopigwa Aprili 2, mwaka huu.

Akizungumza nasi, muda mfupi baada ya kujiunga na kikosi kwenye safari hiyo GSM alisema: “Tunashukuru kwa kuwa kikosi chetu kimefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya mashindano haya lakini tunajua mchezo wetu dhidi ya TP Mazembe utakuwa mgumu na muhimu.

“Tunataka kushinda mchezo huu lakini kwa nafasi ya pekee tuna malengo ya kushinda ubingwa wa mashindano haya, tunajua sio rahisi lakini tupo tayari kupambana kufanikisha hilo na tunaamini katika ubora wa kikosi chetu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: