Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fiston Mayele hajauzwa na Yanga - Jembe

Mayele Saleh Fiston Mayele hajauzwa na Yanga - Jembe

Tue, 18 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa soka Salehe Ally 'Jembe' amesema kwamba mshambuliaji Fiston Mayele hajauzwa na klabu yake ya Yanga huku akisisitiza kuwa mchezaji huyo amewatumikia Wananchi kwa Mkopo.

Jembe ametoa kauli hiyo baada ya mayele kudaiwa kuuzwa Pyramids ya Morocco na kusema kwamba, Mayele aliletwa Yanga na AS Maniema ya nchini mwao Congo DR kwa mkopo ili kuja kuitumikia klabu ya Yanga akitokea AS Vita ya nchini DRC ambako pia alikuwa kwa mkopo.

"Mayele yajauzwa na AS Vita wala Yanga, ameuzwa na timu moja inaitwa AS Maniema ya Congo, ndiyo timu yake ambayo ilimleta Yanga kwa mkopo, kupitia mmiliki wa hiyo timu ambaye ni Jenerali ambaye pia alikuwa kiongozi wa AS Vita.

"Maniema ndiyo timu aliyotoa Maxi Nzengeli, watu wanachanganya vitu, Mayele hakutoka AS Vita alitoka Maniema na ndiyo timu inayomuuza sasa kwenda huko kwingine.

"Mkopo wa mchezaji una wigo mpana na unatoa fursa kwa timu kuelewana kwa namna tofauti. Mkopo wa Mayele Yanga walilipa pesa ya usajili ambayo kiasi kidogo walilipa klabu na kiasi kingine wakamlipa mchezaji lakini hawapati umiliki wa yule mchezaji kwa asilimia 100, umiliki unabaki kwa ile klabu.

"Mkopo kwa mchezaji sio dhambi, Baleke yupo Simba kwa mkopo na hsikii Simba wakikana kwa sababu ni utaratibu wa kisoka dunia nzima.

"Lazima Mayele awaheshimu Yanga kwa kumpa jukwaa la kuonekana Afrika, mafanikio ya Mayele yametokana na vitu vingi ndani ya timu mpaka benchi la ufundi, ushirikiano na wachezaji wenzake na mambo mengine.

"Taarifa nilizo nazo ni kwamba uongozi wa Maniema wamekubali kuchukua pesa kidogo na pesa nyingi wapewe yanga kwenye mauzo ya Mayele. Sijajua kule kama wanamuuza moja kwa moja au wanamtoa tena kwa mkopo, ndiyo maana nilisema mimi si mwendawazimu, narudia Mayele yupo Yanga kwa mkopo," amesema Jembe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: