Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fei Toto kwenda Azam amepotea - Shabiki Simba

Fei Toto Azam Domo Fei Toto kwenda Azam amepotea - Shabiki Simba

Thu, 31 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki kindakindaki wa Klabu ya Simba, Mzee Yusuph Mwenda amesema iwapo angepata cheti basi angeifundisha Azam FC bure bila kuhitaji pesa yoyote kwa sababu imekuwa ikisajili vizuri lakini haipati mataji wala kufanya vizuri.

Mzee Mwenda amesema hayo wakati akizungumzia kitendo cha kiungo Feisal Salum Abdallah 'Fei Toto' kuondoka Yanga kwenda Azam Fc ni kushusha ubora wake na hivi karibuni ataporomoka kabisa na ndiyo maana Kocha wa Timu ya Taifa 'Taifa Stars' Adel Amrouche amemuacha katika kikosi chake kilichoondoka jana kwenda Tunisia kujiandaa na mchezo wa kufuzu AFCON 2023 dhidi ya Algeria.

“Viungo waliowekwa ni wazuri, anayepinga ni u-Yanga na u-Simba, alitaka awekwe nani? Fei Toto hakuna alichokionesha, amekwenda Azam FC kupoteza mpira wake.

“Domayo alitoka Yanga akiwa wa moto akaenda Azam, Ramadhani Singano Messi alitoka Simba akiwa wa moto akaenda Azam walipofika kule nini kilitokea? Walipotea.

“Fei kaenda Azam kuchukua pesa, pamoja na umri wake, kiwango chake kinakwenda kuporomoka. Ndiyo maana Azam inakuwa na wachezaji wazuri lakini haifanyi vizuri kwa nini? Watu hawajiulizi. Ningepata cheti ningeifundisha Azam bila sitaki hata wanilipe,” amesema Mzee Mwenda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: