Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fei Toto kurejea Yanga baada ya kutoka Timu ya Taifa?

FEI TOTO MS.jpeg Fei Toto

Wed, 22 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama ulikuwa hujui basi nikujuze kuwa suala la kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' na klabu yake ya Yanga halijakwisha na litaisha pale tu mchezaji huyo atakaporejea kambini kuungana na wenzake.

Kwa sasa Feisal ameungana na wachezaji wenzake katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ambacho kilitua nchini Misri siku ya jana.

Viongozi wa Yanga wamekuwa na mazungumzo na mchezaji huyo wakimtaadharisha na kumtaka arejee na kam ni masuala ya maslahi yake basi watayaweka sawa pindi atakaporejea kikosini.

Ni takribani miezi mitatu sasa tangu Feisal aondoke Jangwani akishinikizakuvunja mkataba wake ambao unatarajiwa kumalizika mwezi May 2024.

Yanga walizima jaribio lake la kutaka kuvunja mkataba huku wakimfungulia mashtaka mchezaji huyo kwa kupeleka shauri hilo TFF na maamuzi yalieleza wazi kuwa Feisal ni mchezaji halali wa Yanga akiwa na mkataba halali na Yanga.

Fununu zinaeleza kuwa Feisal anaweza kurejea kikosini baada ya majukumu ya timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' na ataungana na baadhi ya wachezaji wenzake wa kikosi cha Yanga waliko pamoja.

Tangu mchezaji huyo ameondoka kikosini bado Yanga imekuwa ikipata matokeo na soka safi likichezwa na hivyo Wananchi wamekuwa hawamzingatii sana.

Ikumbukwe kuwa kama Feisal ataendelea kuweka mgomo basi anaweza kukumbana na adhabu kali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: