Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fei Toto alivyoibadilisha Yanga

Yanga Fei Toto Khd Fei Toto alivyoibadilisha Yanga

Tue, 20 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Aliyekuwa kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi amefunguka akizungumza na Mwanaspoti akisema kukosekana kwa kiungo mshambuliaji aliyekuwa staa wa timu hiyo, Feisal Salum 'Fei Toto' kulimfanya pia abadilishe mfumo wa timu aliokuwa akiutumia wakati kiungo huyo aliyetua Azam alipokuwa akiitumikia timu kabla ya kuweka mgomo baridi.

"Mabadiliko mengine yalitokana na kumkosa Feisal (Salum), alikuwa mchezaji muhimu aliyekuwa anatengeneza uwiano mzuri kati ya viungo na safu ya ushambuliaji. Tulipoanza kumkosa hili nalo lilitupa kazi ya kubadili mambo mengi juu ya muundo wa timu yetu hasa kimbinu," anasema Nabi na kuongeza;

"Changamoto kubwa ilikuja kuondoka kwake kulikuwa katikati ya mashindano, ilihitaji akili ya haraka kuweza kupata muafaka wa kipi kifanyike ili timu isipoteze ubora wake hatua ambayo haikuwa rahisi lakini tukafanikiwa."

Fei Toto sasa ni mchezaji rasmi wa Azam huku Nabi akihusishwa kutua Kaizer Chiefs.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: