Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fei Toto: Nimeondoka Yanga kwa sababu ya manyanyaso

IMG 4201.jpeg Feisal Salum

Thu, 1 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kimya kingi kina mshindo Mkuu kama wasemavyo waswahili. Na hatimaye hii leo Kiungo wa Yanga Feisal salum ameweka wazi sababu ya yeye kuamua kutaka kuvunja Mkataba na Klabu hiyo ya Mitaa ya Jangwani.

Feisal anasema kuwa sababu kubwa sio maslahi kama wengi wanavyodanganyana na kuaminishana mitaani na katika mitandao ya kijamii ikiwemo vyombo vya habari.

Feisal amesema kuwa sababu kubwa ya yeye kutaka kuondoka yanga ni kukithiri kwa manyanyaso aliyokuwa akifanyiwa.

"Kwanza niwape pole mashabiki wa Yanga kwa kuwa walikuwa na imani na mimi na mimi mpaka sasa nina imani nao, labda watu wengi hawafahamu kwa nini naondoka Yanga ama kwa nini nahitaji kuvunja nao Mkataba"

"Sababu kubwa hasa ni kukithiri kwa manyanyaso niliyokuwa nikifanyiwa nikiwa klabuni hapo, kwa hiyo inafikia hatua unaona bora niwape stahiki zao kisha nitafute mahala pengine ama nifanye mambo mengine kwa amani, baadhi ya viongozi walikuwa wakinishutumu kuwa nauza mechi na wanamshambulia mpaka mzazi wangu"

Japokuwa katika hoja yake ya manyanyaso Feisal hakuweka wazi sana ni manyanyaso ya namna gani aliyokuwa akifanyiwa akiwa Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: