Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fei Toto: Nilienda Yanga kwa ajili ya mapenzi, nilikataa kwenda Simba

IMG 4199.jpeg Feisal Salum akihojiwa na Masoud Kipanya

Thu, 1 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kupiga kimya kwa muda mrefu tangu kuibuka kwa sakata lake la kutaka kuvunja Mkataba na Klabu yake ya Yanga, Kiungo wa Yanga Feisal Salum hatimaye ameamua kufunguka kwa nini anataka kuvunja Mkataba na Klabu ya Yanga.

Wakati waliokuwa wengi wakishauri kuwa alipaswa kusubiri Mkataba wake uishe ndipo adai maslahi mapana, kiungo huyo ameweka wazi kuwa alikataa kujiunga Simba SC kwa dau kubwa akachagua kucheza Yanga.

Akizungumza Feisal kupitia Redio ya Clouds FM Feisal anasema;

"Nafsi yangu ilitamani kwenda kuchezea Yanga, nilikubali kwenda kuichezea Yanga kwa kipato kidogo zaidi ya kile ambacho nilikikataa Simba SC, ni kwasababu ya mapenzi tu"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: