Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fei Toto: Niliambiwa nauza mechi

Fei Toto Asd.jpeg Fei Toto

Thu, 1 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Yanga SC, Feisal Salum (Fei Toto) amesema alifikia uamuzi wa kuvunja mkataba na klabu hiyo kutokana na manyanyaso aliyokuwa akiyapata kutoka kwa uongozi, ikiwemo kuzushiwa kwamba ameuza mechi.

Akizungumza kupitia Clouds FM, Fei Toto amesema tangu aliposaini mkataba mpya na Yanga ambao unaisha mwakani, manyanyaso ndio yamezidi na kwamba ada yake ya uhamisho ilikuwa shida na kwamba mshahara analipwa lakini kwa manyanyaso.

"Mimi nimeshalia uwanjani... kiongozi anakutukana 'kama huwezi utarudi kwenu Pemba... lakini nikaendelea kuvumilia," amesema Fei.

Ameongeza kuwa manyanyaso hayo hayakuishia kwake bali yalikwenda hadi kwa mama yake mzazi ikiwemo kumtusi kwa kumuita "Andazi," na kwamba Rais wa Yanga, Mhandisi Hersi Said anawaaminisha watu kwamba Fei Toto ni mbaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: