Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fei Toto: Muda ukifika nitaanika kila kitu

Feisal Salum Fei Toto Malengo Fei Toto

Sat, 15 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati uongozi wa Yanga ukimwita mezani kiungo, Feisal Salum 'Fei Toto' ili kumaliza sakata lake, nyota huyo amesema muda sahihi ukifika ataweka wazi mambo yote yanayoendelea kuhusiana na uamuzi wa kutaka kuachana na klabu hiyo ambayo ameufanya.

Fei Toto amesema hivyo jana ikiwa ni siku mbili zimepita baada ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kusema itatoa uamuzi wake ifikapo Mei 4, mwaka huu.

Kiungo huyo aliliambia gazeti hili kwa sasa anasubiri kamati imalize kikao chake na kutoa hukumu, lakini muda muafaka ukifika atazungumza mambo yote muhimu hadharani.

"Muda ukifika nitazungumza, muda sahihi ukifika nitaweka kila kitu wazi," Fei Toto alisema kwa kifupi.

Naye Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga, Simon Patrick, amesema wanamkaribisha mchezaji huyo kufanya mazungumzo na si kupitia njia nyingine tofauti.

Simon alisema Yanga hawamng'ang'anii nyota huyo lakini wanataka utaratibu ufuatwe, wakiruhusu mchezaji kuondoka kwa njia hii hakutakuwa mpira kwa sababu kila mchezaji ataamka asubuhi na atasema hana furaha basi anaondoka.

“Huu ni uhuni, hautakiwi kuruhusiwa katika mpira wetu, ziko njia rasmi za kuvunja mkataba na zinafahamika hadi Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA), tunachotaka kanuni za mpira zisimamiwe, tusiruhusu maharamia wanaotumia fedha. Hii si kwa Yanga tu, ni klabu zote,” alisema mkurugenzi huyo.

Aliongeza Yanga wanataka kuona sheria na taratibu zinafuatwa, kamwe hawawezi kumruhusu aondoke kiholela kwa maslahi ya heshima ya klabu.

“Yanga ilitoa taarifa kama kuna timu inamhitaji nyota huyo basi wafike katika ofisi zetu na Fei Toto mwenye aje kukaa meza moja ili kuvunja huo mkataba,” aliongeza.

Nyota aliwasilisha shauri la kutaka kuvunja mkataba wake na Yanga kwa kulipa kiasi cha Sh. milioni 112 kama mkataba wake ulivyosema, lakini klabu hiyo ilikataa na kufungua kesi TFF.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: