Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fei Toto: Mnamfananisha mama yangu na andazi?

Mama Wa Feisal Azungumza Fei Toto: Mnamfananisha mama yangu na andazi?

Thu, 1 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, feisal Salum 'Fei Toto' amesema kuwa mama yake mzazi amedharirishwa na baadhi ya viongozi wa klabu hiyo kwa kufananishwa na andazi.

"Mama yangu mimi ndio pepo yangu, mnamfananisha mama yangu na andazi halafu mimi nikubali tu, je, ingekuwa ni wewe mama yako anafananishwa na andazi, je, wewe ungekubali kitu kama hicho.

“Kauli aliyoisema mama yangu kuwa nilikuwa nakula ugali na sukari alimaanaisha kipindi cha nyuma na ni kweli kila mmoja anajua tulipitia kipindi kama hicho nyuma, sasa kwanini wamtukane mama yangu.

“Mimi nilikaa meza moja na rais na makamu wake nikamwambia hapa tulipofikia panatosha siwezi kuendelea sasa akisema mimi sijakaa kuzungumzanao sielewi.

“Nilisaini mkataba mpya kwa lugha ya kingereza tulikubaliana kuongeza miaka miwili lakini kumbe kwenye makataba wameandika miaka mitatu mimi nikasaini

“Mimi sikuwa na mwanasheria hapo awali sielewi lugha ya Kingereza walienda nje ya makubaliano ambayo tuliyafanya kwa mdomo tulikubaliana miaka miwili wao wakaandika miaka mitatu mimi nikasaini bila ya kujua.

“Kwa sasa nimeona umuhimu kuwa na wanasheria na wameniambia mikataba lazima uwe kwa lugha ya Kiswahili," Feisal Salum.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: