Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamu mbinu za Marumo vs ubora wa Yanga

Yanga Marumooo (14).jpeg Magazeti

Tue, 9 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachambuzi wa soka nchini kupitia East Afrika Radio wwmedokeza kwa ufupi kuhusu mfumo wanaotumia Marumo Gallants chini ya kocha wao Dylan Kerr katika kushambulia huku wakiwa si wazuri sana kujilinda.

"Marumo Gallants ikija kwako itakubali kipigo lakini siyo kikubwa. Siwaweki kuwa ni timu tishio kwa Yanga, lakini kwa ubora wa kikosi chao, wachezaji wanakimbia sana na mipira yao mirefu wanapaswa kuchungwa.

"Mshambuliaji wao Chivaviro ni mzuri sana, ni mchezaji ambaye anaweza kuifunga timu yoyote na wakati wowote, japo Mayele ni mzuri zaidi kutokana na 'Class' aliyokuwa nayo" Amesema @justinekessytz kupitia kipindi cha #Kipenga cha #EastAfricaRadio.

"Marumo Gallants ni timu ambayo inafunga magoli mengi siyo kwa bahati mbaya, pia nayo inaruhusu magoli. Wanacheza mpira wa direct, mpira wa kushambulia na wanapoondoka huwa wanaacha nafasi, ni kazi ya kocha Nabi sasa kujipanga kushambulia"

"Nawaona Marumo wao hawajabalance lakini Yanga wamebalance kwenye maeneo mengi. Yanga wanaweza kushindana nao kwenye kiungo na hata ulinzi. Hii ni mechi ya kimkakati kwa Yanga, muda mwingine huitaji kuwa bora ili kupata matokeo" Amesema @ibrakasuga kupitia #Kipenga ya #EastAfricaRadio.

Ikumbukwe kuwa, katika michezo 8 kuanzia makundi mpaka robo fainali, Marumo wamefunga mabao 14 na kuruhusu kufungwa mabao 11 wakati Yanga wamefunga mabao 11 na kuruhusu kufungwa mabao 4 pekee. Yanga wana cleansheets 5, Marumo cleansheets 2.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: