Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamu kanuni ngumu za mashindano ya Super League

Tshabalala Ahly Fahamu kanuni ngumu za mashindano ya Super League

Thu, 14 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashindano ya African Football League yanatarajia kuanza kurindima kwa mechi ya ufunguzi katika Dimba la Mkapa kati ya Simba Sc dhidi ya Al Ahly ya Misri mnamo Oktoba 20, 2023.

Ni timu nane pekee ambazo zitamenyana kwenye msimu wa kwanza wa mashindano hayo ya kihistoria huku mkwanja mrefu ukimwagwa kwa timu itakayoshiriki mashindano hayo.

Timu nane zitakazoshiriki ni Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Al Ahly ya Misri, Wydad Casablanca ya Morocco, Esperance ya Tunisia, TP Mazembe ya Vongo DR, Enyimba FC ya Nigeria, Simba SC ya Tanzania na Petro Atletico ya Angola.

Miongoni mwa kanuni za mashindano hayo ni kwamba; Klabu yoyote kati ya 8 itakayoamua kujitoa katika Ligi ya Soka ya Afrika mwaka huu itapigwa faini ya kati ya Dola 15,000 hadi Dola 20,000 na kufungiwa kushiriki mashindano ya mwaka ujao.

Wachezaji 30 watasajiliwa kwa kila klabu.

Wachezaji 23 watatajwa kwenye jedwali la timu siku za mechi.

Wachezaji 11 wa kuanza mchezo.

Wachezaji 12 watakuwa kwenye benchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: