Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamu: Yanga ndiyo klabu iliyomleta Chama nchini Tanzania

Lwandamina Dfs Fahamu: Yanga ndiyo klabu iliyomleta Chama nchini Tanzania

Tue, 25 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga ndio klabu ya kwanza kumleta mchezaji Clatous Chota Chama raia wa Zambia katika ardhi ya Tanzania.

Picha ya kwanza ni Clatous Chota Chama akiwa Tanzania kwa mara ya kwanza, alipiga picha hii na Omar Kaaya wakati huo akiwa kiongozi wa Yanga wakati kocha mkuu akiwa George Lwandamina raia wa Zambia.

Kuna kiongozi wa Simba hivi karibuni alikaririwa akisema kwamba yeye ndiyo chanzo cha Chama kucheza kwenye Timu yao ila ukweli huu hausemwi Chama Tanzania aliletwa na Yanga SC.

Hakuna Kiongozi wa Simba SC aliyemleta Chama hapa Tanzania, Chama aliletwa na George Lwandamina wakati huo akiwa Kocha wa Klabu ya Yanga lakini kutokana na ukata wa pesa waliokuwa nao Yanga SC ikashindwa kumsajili na hapo Simba wakapata mwanya na kumsajili chini ya mtaalam Hans Poppe huku Magori akiwa kama msaidizi.

Wanachama wa Klabu ya Yanga wanadai kuwa ikitokea Yanga ikamsajili Chama siyo ajabu maana ni kama inamchukua tu mchezaji wake ambae hapo awali aliwahi kuwa kwenye mipango ya Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: