Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FCC 'yamkataa' Mo Dewji sakata la mabadiliko Simba

Mohamed Dewji Mo Dewji FCC 'yamkataa' Mo Dewji sakata la mabadiliko Simba

Wed, 2 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji kudai kuwa wapo baadhi ya viongozi ndani ya Simba wanakwamisha mchakato wa mabadiliko wa klabu hiyo, Tume ya Ushindani (FCC) imeibuka na kujibu hoja ya mfanyabiashara huyo.

Akitolea maelezo ya kina kuhusu sakata linaloendelea la mpango wa uwekezaji kati ya Simba na mwekezaji wao Mo, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC), William Erio, amesema watu wengi wanazingatia zaidi upande wa Mwekezaji na kusahau kuhusu majukumu ya Klabu ya Simba.

Erio alisema, “Baada ya kukamilisha masharti ya Mwekezaji na ya Simba, tuliutoa cheti kuwa muungano umepitishwa na kile ambacho kilikuwa kinaombwa kimeridhiwa, na sasa kinachofuata ni utekelezaji.”

Aidha, aliongeza, “Wiki mbili zilizopita, upande wa Klabu (Baraza la Wadhamini wa Klabu) walitakiwa kufika RITA (Wakala wa Usajili, Ufilisi, na Udhamini) ili kuhakikisha Hati za Jengo la Klabu zote zinakuwa mali ya Simba Sports Club Limited. Hata hivyo, sina taarifa kamili kuhusu jinsi mambo yalivyosonga mbele kuhusu suala hilo.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: