Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Exclusive: Namba 6 wa Yanga mwamba huyu hapa!

Pacome Asec 1).jpeg Pacome Zouzoua.

Tue, 18 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yule mchezaji anatangazwa kwa nguvu kubwa na Yanga kuwa ndiye mrithi wa Feisal Salum Abdallah 'Fei Toto' tayari ameshafahamika mpaka sasa.

Sio siri tena, kiungo fundi Zouzoua Pacôme (26) ndiye anatajwa kuwa ndiye anatarajiwa kutambulishwa muda wowote baada ya usajili wake kukamilika na atapewa jezi namba 6 ambayo imekuwa ikiimbwa na upngozi wa klabu hiyo.

Chanzo chetu kutoka ndani ya Yanga kimeihakikishia Tanzaniaweb.com kuwa, Pacome kutoka Asec Mimosas tayari ameshamalizana na Yanga na yupo nchini, hivyo muda wowote anatambulishwa kwa Wananchi ili kijiunga na wachezaji wenzake kambini Avic Town.

"Ni kweli tumeshamalizana na Pacome, huyu ni mtu na nusu, fundi wa mpira. Siwezi kusema lini atatambuloshwa lakini muda wowote kuanzia sasa ataanikwa kwenye page za Yanga na mtamuona," kimesema chanzo hicho.

Pacome ndiye mchezaji bora wa Asec Mimosas ya Ivory Coast wa msimu uliomalizika akiwashinda Kwame Kramo ambaye amesajikiwa Simba Sc, Mohammed Zoungrana na beki Yao Kouas Attohoula ambaye amesajiliwa Yanga.

Pacome ambaye ni raia wa Ivory Coast anacheza nafasi ya kiungo mshambuliaji namba 10 na namba 8 pia kama alivyokuwa Fei Toto.

Awali akihojiwa kuhusu mchezaji atakayevaa jezi namba sita iwapo atakuwa beki au mshambuliaji, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe alisema;

“Ukiangalia tulianza na mabeki, tukaja viungo na tumetambulisha winga kwa hiyo maana yake haturudi nyuma tena.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: