Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Edo Kumwembe: Mkude ni zaidi ya Mzamiru, Kanoute pale Simba

Edo Mkude Edo Kumwembe: Mkude ni zaidi ya Mzamiru, Kanoute pale Simba

Fri, 21 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati bado kukiwa na kitendawili kuhusu kuagwa kwa aliekuwa kiungo mwandamizi wa Klabu ya Simba SC Jonas Mkude na Klabu yake ya zamani baada ya kuachwa na hasa ni baada ya Mkude kusajiliwa na Yanga ambao ni wapinzani wa jadi wa Simba.

Kitendo tu cha Mkude kuachwa na Simba kiliibua mjadala huku wengine wakisema Mkude hajaisha kiasi cha Simba kuamua kuachana nae bali pengine kulikuwa na sababu nje ya Uwanja.

Sasa Mchambuzi mkongwe wa michezo nchini, Edo Kumwembe ametoa maoni yake kuhusiana na ubora wa mchezaji huyo na kitu cha kufanya ili arudi katika ubora wake wa hali ya juu aliokuwa nao hapo awali kwani viungo aliowaacha kikosini hakuna anaemfikia kwa uwezo kama ataamua kupambana nao.

Akizungumza Edo anasema;

“Binafsi naamini kwamba Jonas Mkude ana kipaji kikubwa kuliko Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin, tofauti pekee katika miezi (24) iliyopita ni kwamba wao wamejituma zaidi kuliko Mkude. ”

“Hatujui kilichotokea katika maisha yake binafsi, lakini ukweli ni kwamba soka la Jonas Mkude lilikwenda chini na wenzake wakanyanyua zaidi vipaji. Na sasa ni jukumu la Mkude kuhakikisha kwamba anaokoa kipaji chake, ”

Je Mwanasimba unakubaliana na maoni ya Edo Kumwembe?Tupe maoni yako

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: