Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Edo Kumwembe: Kwa hili, Simba jifunzeni kwa Yanga

Taibi Lagrouni. Taibi Lagrouni.

Thu, 31 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi maarufu wa masuala ya Soka katika Kituo cha Wasafi Media, Edo Kumwembe amesema kuwa kikosi cha Yanga SC kwa sasa kinabebwa na 'level ya fitness' (utimamu wa kimwili) mkubwa ambao wanao kuzidi vilabu vingi nchini, ndiyo maana wana pumzi na nguvu ya kutosha kupambana mwanzo mpaka mwisho wa mechi.

Edo amesema hayo mara baada ya kushuhudia michezo mitatu mfululizo Yanga ikifunga mabao matano kila mchezo jambo ambalo halijawahi kutokea kwenye timu za Tanzania kwa miaka mingi na kuwataka vilabu vyote vya Tanzania wakiwemo Simba kujifunza kutoka kwa Yanga.

“Mabao 15 katika mechi 3 na ni mfululizo, si bahati mbaya. Kuna mabao ambayo yapatikana kwenye mechi ambayo yanatokea tu tu kwenye nafasi, lakini Yanga wanatoa presha kubwa sana kwa wapinzani kiasi kwamba unalazimika kutoa mabao hayo. Yanga wanacheza mpira mkubwa na kumlazimisha adui afanye makossa.

“Haya yote ni kwa sababu Yanga wapo fiti sana, achana na uwezo wao, sijui wanafanya nini kule Avic Town Kigamboni, sisi hatujui lakini ninachojua ni kwamba wana kocha bora sana wa fitness ambaye wamemtoa RS Berkane iliyokuwa bingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika.

“Yule Manywele (Profesa Helmy Gueldich) ilionekana huyu wa sasa (Taibi Lagrouni) ni mzuri zaidi, wachezaji wa yanga wanasema huyu jamaa ni mzuri sana, tazama bao alilofunga Max Nzengeli dhidi ya JKT Tanzania, amepiga mpira kipa akaurudisha, akaenda tena akavuka mabeki akashuti kwa nguvu akafunga, unaona kabisa vijana wana fitness ya hali ya juu.

“Yanga sasa sisi hawataki mpinzani akae na mpira, ukiwanyang’anya tu muda huo huo wanakuja kwa nguvu kuutaka mpira wao. Kwa hiyo timu nyingine zijifunze kwa Yanga, sio suala la kipaji na uwezo tu lakini fitness ni muhimu sana kwenye soka la leo,” amesema Edo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: