Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dodoma Jiji yakataa kuwa daraja la ubingwa Yanga

Dodoma Jiji Manusura Dodoma Jiji yakataa kuwa daraja la ubingwa Yanga

Fri, 12 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongzoi wa Dodoma Jiji umeweka wazi kuwa wanahitaji pointi tatu muhimu dhidi ya Yanga ambao watacheza nao Mei 13, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Dar.

Dodoma Jiji ipo nafasi ya 10 baada ya kucheza mechi 27 ina pointi 31 na Yanga ambaye yuko kileleni na alama zake 71 kama akishinda mchezo huo basi atakuwa bingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Akizungumza nasi, Moses Mpunga alisema kuwa, wanatambua juu ya mchezo wao dhidi ya Yanga na wapo tayari kupata pointi tatu muhimu.

“Mchezo wetu dhidi ya Yanga ni muhimu kushinda kwa kuwa tunahitaji pointi tatu, tunatambua ni timu imara inafanya vizuri kwenye mashindano ya ndani nay ale ya kimatafa lakini tumejipanga.

“Ilikuwa hatujajua siku ya kucheza nao lakini kwa sasa ratiba ipo wazi hivyo inatufanya tuwe tayari kuikabili timu hiyo na wachezaji wapo tayari kwa mchezo wetu mgumu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: