Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dodoma Jiji wamuwinda Mlinzi wa Yanga

Bryson Yanga' Mlinzi wa Yanga David Bryson (kulia)

Sat, 24 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa wa KMC FC umeanza mazungumzo ya kimya kimya ya kumrejesha aliyekuwa beki wa kushoto wa timu hiyo, David Bryson ambaye mkataba wake wa miaka miwili na Young Africans unafikia tamati mwishoni mwa mwezi huu.

Nyota huyo alijiunga na Young Africans Agosti mwaka 2021 akitokea KMC FC ambako alionyesha kiwango kizuri na kuzivutia timu nyingi ingawa tangu amejiunga na mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara mambo yamekuwa ni magumu.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya timu hiyo kimeeleza kuwa, Bryson licha ya kutopata nafasi ya kucheza ila bado ni mchezaji mzuri na anaweza kujiunga nao kama mambo yataenda sawia.

“Tunatarajia kukutana hivi karibuni kujadili mambo mbalimbali ya timu kwa ajili ya msimu ujao, suala la Bryson siwezi kusema ni kweli au laah! Hivyo tusubirie kwanza,” kimesema chanzo hicho.

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema tayari alishakamilisha ripoti yake kwa ajili ya msimu ujao na kazi iliyobaki ni kwa viongozi kumtimizia mahitaji yake.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa timu hiyo, Daniel Mwakasungula alisema walikutana jana kujadili msimu mzima ulivyokuwa ikiwemo usajili mpya na hatima ya kocha wao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: