Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Djuma Shabani afunguka Wakongo wanachofanyiwa Yanga

DJUMA MOLOKO Djuma Shabani afunguka Wakongo wanachofanyiwa Yanga

Wed, 5 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa Yanga Djuma Shabani, ambaye ana mkataba na timu hiyo mpaka 2024, amesema ana furaha sana kucheza soka la Tanzania kwa sababu viongozi wa soka wanajua kuwahudumia vyema wachezaji.

Djuma Shabani amezungumza na mwanahabari wa umoja wa wachezaji wa Congo Ufs, Olivier Sefu na kumwambia wachezaji wa Kitanzania hawana matamanio tena ya kuja kucheza Congo DR kama enzi za Mbwana Ally Sammata.

Amesema ligi ya Congo- DR inatia hofu kwa sababu inakosa wasimamizi makini na uratibu mzuri wa ligi huku wachezaji wakipitia kipindi kigumu na kusema kama hawatabadilika basi wasiwe na matumaini yoyote. 

Amesema Tanzania ligi haisimami hovyo kama Congo ambako amesema viongozi wana vipaumbele vyao na wala hawachukuliwi hatua huku akipigilia msumari kuwa Tanzania kila klabu inanufaika na haki za matangazo ya televisheni na akiisifu ligi ya Tanzania kuwa na hadhi ya juu kwa kushika nafasi ya 5.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: