Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Djuma Shaban hatihati kuwakosa Marumo Gallants

Cheickan Diakite X Djuma Shaba Djuma Shaban hatihati kuwakosa Marumo Gallants

Tue, 9 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi amesema kuwa huwenda beki wake wa kulia Djuma Shaban akaikosa mechi ya kesho ya nusu fainali dhidi ya Marumo Gallants utakaopigwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya kesho.

Sababu ya Djuma Shaban kuwa katika hatihati ya kuikosa mechi hiyo ni kutokana na kusumbuliwa na mafua nlyaliyopelekea kushindwa kufanya mazoezi na wenzake.

“Wachezaji wana ari ya juu, tumejiandaa kikamilifu kulingana na tulivyomsoma mpinzani wetu, tupo tayari kupambana, kujituma na kuhakikisha tunapata matokeo nyumbani. Tutacheza kwa akili sana na contentration ya juu.

“Wachezaji wetu wote wako fiti kucheza mechi ya kesho, kasoro Djuma Shabani ambaye hajafanya mazoezi ya jana sababu ya mafua, bado tunamtazama kama tutaweza kumtumia, lakini wengine wote wapo fiti,” amesema Nabi.

Aidha, Nabi amewataka mashabiki kutokata tamaa wakiwa uwanjani, washangilie mwanzo mwisho dakika 90 kama wanavyofanya mashabiki wa timu za Uarabuni kule mbele, hata kama mchezaji akikosea basi wamshangilie ili kumrudisha mchezoni na kumpa sapoti ili ajitume zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: