Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dickson Job ampagawisha Nabi

Dickson Job Modern Footballer Dickson Job

Fri, 23 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Kocha Nabi akitua Yanga kuna wachezaji kadhaa alitambulishwa na nafasi zao kikosini lakini katika wote ni Mlinzi Dickson Job ndio aliemshangaza Mtunisia huyo.

Katika mahojiano yake na chombo kimoja cha habari Nabi amedokeza kuhusiana na hilo ambapo anasema kuwa;

Kama kuna mchezaji aliyenishangaza juu ya kipaji chake basi ni Dickson Job, wakati nafika na nilipoambiwa anacheza beki wa kati nilisubiri kuona ana kitu gani cha ziada lakini alinijibu kwa vitendo uwanjani, huyu ni kijana mdogo ambaye ana akili kubwa sana anapokuwa uwanjani.

Job hajui kukataa jukumu unalomtuma amekuwa ni rahisi kwake kubadilika wakati wote, ana nidhamu kubwa ni sawa na wale rafikizake Kibwana na mwanangu Mshery bahati mbaya aliumia lakini ni kipa mzuri, kwa Job ni bahati mbaya sana anacheza soka Tanzania.” - amesema Kocha Nabi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: