Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diarra, Musonda nao kuondoka Yanga

Diarra Musondaaa Diarra, Musonda nao kuondoka Yanga

Sun, 5 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Straika wa Yanga, Kennedy Musonda na kipa Djigui Diarra wameongeza idadi ya wachezaji wa Young Africans walioitwa kwenye timu zao za taifa.

Avram Grant aliepewa ridhaa ya kukinoa kikosi cha Zambia "Chipolopolo" amemjumuisha mshambuliaji wa Yanga Kennedy Musonda kwenye timu yake wanapoenda kucheza michezo miwili ya kufuzu Kombe la Mataifa Afrika dhidi ya Lesotho.

Nae mlinda lango nambari moja wa Young Africans, Djigui Diarra ameitwa tena kwenye kikosi cha miamba ya Afrika Magharibi, Mali ambao wanaenda kucheza michezo miwili dhidi ya Gambia kwenye kuwania kufuzu kwenda Kombe La Mataifa Afrika (AFCON).

Kuitwa kwa wachezaji hao kunafanya idadi ya wachezaji wa Yanga walioitwa kwenye timu zao za Taifa kufikia wanne mpaka sasa ambapobwengine ni mshambuliaji Fiston Mayele (Congo DR) na kiungo mshambuliaji Stephane Aziz KI (Burkina Faso).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: