Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dabi ya Kariakoo; Kitawaka!

MUSONDA CHAMA DF Dabi ya Kariakoo; Kitawaka!

Sat, 15 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea Kariakoo Dabi, vita kubwa inayosubiriwa kutamwa na mashabiki ya mabeki na washambuliaji wa Simba watakapoonyesheana umwamba.

Dabi hiyo inayotarajiwa kujaa upinzani mkubwa, itapigwa kupigwa kesho Jumapili saa kumi na moja jioni kwenye Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, Simba wataingia uwanjani kibabe kwa ajili ya kutaka kulipa kisasi cha kufungwa mara mbili mfululizo walizokutana katika Ngao ya Jamii.

Mara zote hizo mbili, Simba wamefungwa na mfungaji mmoja pekee ambaye ni Fiston Mayele ambaye katika mchezo wa kwanza wa Ngao ya Jamii walioucheza msimu uliopita aliwafunga bao moja katika ushindi wa mabao 1-0.

Aliwafunga tena katika Ngao ya Jamii ya msimu huu akifunga mabao mawili pekee katika ushindi wa bao 2-1 huku hilo la Simba likifungwa Pape Sakho.

Kuelekea mchezo huu, vita kubwa itakuwepo kati ya Mayele na mabeki wa Simba watakaoongozwa na Hennock Inonga, Joash Onyango, Mohammed Ouattara na Kennedy Juma hawatakubali kumuachia mshambuliaji huyo ateteme watakutana.

Wakati mabeki hao wa Simba wakijipanga kumzuia Mayele ambaye ndio kinara wa mabao katika ligi akifunga 16 mwenyewe ameandaa mbinu za kuibomoa ng’ome hiyo ya ulinzi ya Simba inayonolewa na Mbrazili Roberto Oliviera ‘Robertinho’.

Pia mabeki wa Simba watakutana na sapraizi ya Mzambia Kennedy Musonda ambaye yeye ndio dabi yake ya kwanza kuicheza tangu ajiunge na Yanga katika dirisha dogo la usajili.

Robertinho ana kibarua kigumu cha kuiandaa safu yake ya ulinzi, kwani washambuliaji wote wa Yanga wana kasi wanapokuwa mpira wakikokota mipira Mayele, Musonda pamoja na viungo wake Stephane Aziz Ki na Jesus Moloko aliyekuwepo katika kiwango bora hivi sasa.

Kwa upande wa mabeki wa Yanga na washambuliaji wa Simba, moto utawaka kwelikweli kutokana na ubora wa kila idara.

Mabeki wajiandae kukutana na sapraizi ya mshambuliaji mpya wa Simba, Mkongomani Jean Baleke ambaye yeye kwa mara ya kwanza ataicheza dabi hii.

Safu ya ulinzi ya Yanga itakayoongozwa na nahodha Bakari Mwamnyeto, Dickson Job na Ibrahim Bacca ambaye ingizo jipya katika kikosi cha kwanza cha Mtunisia Nasreddine Nabi.

Walinzi wa Yanga hawatakiwi kufanya makosa ndani na nje ya 18 ya goli, kutokana na ubora ambao Baleke mwenye mabao saba akiwa na msimu wake wa kwanza baada ya kusajiliwa dirisha dogo.

Baleke ndiye mshambuliaji tishio na hatari hivi sasa katika kikosi cha kwanza ambaye ni mzuri katika kufunga kichwani na mguuni, mabeki wa Yanga hawatakiwi kumuachia katika eneo lao hatari.

Yanga pia wanatakiwa wamchunge kiungo mshambuliaji wa Simba Mzambia, Clatous Chama ambaye ni hatari wa kupiga pasi za mwisho na kufunga, kama wakimsahau basi Baleke hatawaacha salama.

Yupo kiungo mwingine wa kuchungwa Mrundi, Saidi Ntibanzonkiza ‘Saido’ ambaye yeye ni hatari anayeiitaji uangalizi mkubwa ambaye katika msimu hu amehusika mara 19 katika mabao akipiga asisti 9 huku akifunga 10 ambacho sio kitu kwake, hivyo vita kubwa itakuwepo kati ya safu ya ushambuliaji ya Simba na mabeki wa Yanga katika mchezo huo ambao nyota huyo anaonekana kuitaka mechi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: