Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DIDA: Serikali izisapoti Timu zetu Kimataifa

Deogratius Munish DIDA.jpeg Kipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi 'Dida'

Thu, 14 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi 'Dida' amesema ili timu zetu zifanye vizuri kimataifa inatakiwa Serikali kuwapa sapoti kubwa kwasababu wao ndio mama na baba hapa nchini.

"Mashabiki na wapenzi wa klabu hizi wanapaswa kushirikiana na kuwapa moyo wachezaji wao hii itasaidia kupiga hatua kutokana na umoja wetu,"

Dida ametoa maoni hayo wakati akichangia mada iliyoandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited kwenye mtandano wa kijamii wa X Space iliyokuwa inaeleza nini kifanyike klabu za Tanzania zifanye vizuri kimataifa.

"Changamoto zipo kwenye kila kipindi hasa timu zinapoenda ugenini kwa sababu tunapitia mengi hasa kutokana na itikadi za wenzetu jambo ambalo ni tofauti na kwetu ambapo amani imetawala," Kipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi 'Dida'.

"Ushirikiano bado upo kama zamani na ninafurahia kuona Rais wetu wa nchi, Samia Suluhu Hassan anavyotoa sapoti kwa timu zetu," Kipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi 'Dida'

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: