Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Clement Mzize anajua nyie

Clement Fr Mzize Clement Mzize

Wed, 8 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuaminiwa na kupewa nafasi katika Kikosi cha Timu ya wakubwa mshambuliaji Kinda wa Yanga, Clement Mzize amefanya kweli.

Mzize amekuwa na mchango mkubwa katika Kikosi cha Yanga akifunga na kutoa pasi za magoli katika michezo mbalimbali anayopewa nafasi.

Sasa kutokana na ujio wake mzuri, Straika wa zamani wa Nazareth, Simba na Taifa Stars, Emmanuel Gabriel ‘Batgol’ amemwangalia mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize na kutamka kuwa dogo anajua sana. . “Nimefuatilia pasipo na shaka anatakiwa kuwepo timu ya Taifa, hata kwa kukaa nje ili tuendelee kumtengenezea mazingira ya kujiamini. Hata Kocha wa Stars aambiwe dogo anajua akichaguliwa atazidi kujiamini.” Alisema Gabriel ambaye kwa sasa ni Meneja wa Fountain Gate.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: