Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chilunda aahidi makombe Simba

Shaaban Chilunda 22 23.png Chilunda aahidi makombe Simba

Fri, 11 Aug 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mshambuliaji wa Simba aliyesajiliwa dirisha hili la usajili, Shaban Chilunda amesema kutokana na muunganiko wa timu yao, watachukua kila kombe msimu huu.

Chilunda ambaye juzi alikuwa gumzo kwenye Uwanja wa Mkapa baada ya kupiga picha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema kwa sasa wameimarika na anaiona timu hiyo kwenye kilele cha mfanikio.

Chilunda anadai suala la kupiga picha na Rais ni jambo kubwa kwake kwa kuwa kila siku alikuwa anaomba jambo hilo litokee.

“Kwanza sikutegemea kama tukio kama hili lingetokea kwangu, ilikuwa ni supraizi japokuwa nilikuwa natamani siku moja nipige picha na Rais. Nilishtuka lakini nilifurahi sana hata wenzangu walitamani wangekuwa wao kuona Rais amekaa karibu yao na kuwagusa,” alisema.

Pia staa huyo wa zamani wa Azam, amesema mashabiki watarajie mambo makubwa kutoka kwake na muhimu ni kumwombea ili aweze kufanikisha malengo yake pamoja na wachezaji wenzake.

“Nafahamu mashabiki wanachohitaji kutoka kwetu ni miaka miwili sasa klabu yetu haijapata kikombe chochote, kikubwa watuombee dua watusapoti kwa kila namna ili tuweze kufikia malengo.

“Muunganiko wa timu ndio kila kitu na kama mnavyoona tuna muunganiko mzuri, yapo mengi tunayoyazungumza lakini kubwa zaidi kwa sasa ni kuangalia kile kilicho mbele yetu na Mungu akijalia tutachukua kila kikombe kilichopo mbele yetu.”

Simba imesafiri jana kwenda Tanga kwenye michuano ya Ngao ya Jamii ambayo inaanza leo kwa Yanga kuvaana na Azam FC na kesho watacheza Simba na Singida Fountain Gate na washindi watakutaka kwenye fainali Agosti 13.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: