Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Che Fondoh: Nimekaribishwa Bongo kama shujaa

Zxc Malone Wer Che Fondoh Malone.

Tue, 18 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki mpya wa Simba, Che Fondoh Malone amesema kuwa mapokezi aliyoyapokea nchini Tanzania ni makubwa na ya kuheshimika hivyo ana deni kubwa la kuwafanyia kazi iliyotukuta mashabikiwa Msimbazi.

Malone ambaye amesajiliwa Simba SC hivi karibuni kutokea Cotton Sports FC ya nchini Cameroon akiwa mchezaji bora wa msimu uliopita.

"Nilifurahi sana nilipofika hapa Tanzania kwa sababu nilikaribishwa kama shujaa kwa ukarimu na heshima nyingi.

"Watu wa nchi hii wanapenda soka na wanawaheshimu sana wachezaji wao. Wanawaunga mkono katika nyakati nzuri na mbaya na kuhakikisha mchezaji anatendewa vyema. Hauwezi kuhisi tofauti kati ya mgeni na raia wao," amesema Malone.

Tayari Malone ameshawasili nchini Uturuki kwa ajili ya kujiunga na wachezaji wenzake kwenye mazoezi ya pre-season.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: