Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama ana mengi ya kujifunza kwa Pacome - Kamwe

CHAMA PACOMEE Chama ana mengi ya kujifunza kwa Pacome - Kamwe

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari wa Klabu ya yanga, Ally Kamwe amesema kuwa mchezaji wa Simba Sc, Clatous Chama hajafikia kiwango cha mchezaji mpya wa Yanga, Pacome Zouzoua raia wa Ivory Coast.

Kamwe amesema hayo mara baada ya mjadala kuibuka na kuwafananisha viungo hao wa ushambuliaji kutokana na viwango vyao wanavyovionyesha kwenye Ligi ya Tanzania na soka kwa ujumla.

"Chama na Pacome hawafanani hata kidogo, Pacome ameshavuka level ya kuwa mchezaji wa miguu, yupo kwenye level ya kuwa profesa wa soka na hili jina alipewa tangu mwaka 2013, amepewa gari na TFF ya Ivory Coast huku mashabiki wakimuwekea mafuta.

"Unamfananaisha mtu mwenye kadrigrii na profesa? Ni mbingu na ardhi, Pacome yupo mbali sana. Sijakwambia mataji ambayo Pacome ameshinda wala Ligi alizocheza, msimfananishe na watu wa Visit Kidimbwi.

"Pacome amecheza Ligi ya Ufaransa, level za kawaida ameshavuka yupo kwenye level ya kufundisha mpira akiwa anaucheza. Akiingia uwanjani viungo wengine wanachukua kalamu na karatasi wanaanza kujifunza akiwemo huyo uliyemtaja (Chama).

"Pacome anapiga miguu yote miwili, ana kasi, anaweza kukaba, kuchezesha timu na kufunga anavyotaka, Pacome yupo mbali mno. Haya maneno hayafai kuongelewa mdomoni, subirini aingie uwanjani. Rais wa Asec amesema haya mnayoyaona ni asilimia 30 tu ya fitness yake.

"Hao wachezaji mnaowasema wana ndoto za kuwa kama Pacome, acha muda huu wajifunze kutoka kwa Profesa ashushe vitu," amesema Ally Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: