Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama ampa kazi mbili Baleke

Jean Baleke Tatu Jean Baleke

Sun, 6 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Clatous Chama ana historia mbili tamu ambazo zote zinaweza kufikiwa na Jean Baleke au mojawapo isifikiwe wakati Simba itakapokabiliana na Power Dynamos katika kilele cha Tamasha la Simba Day kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Mkapa.

Historia ya kwanza ya Chama ambayo inaonekana ni rahisi kwa Baleke kuifikia ni ile ya kucheza mechi ya kilele cha tamasha hilo akiwa na Simba pia akiwa na kikosi cha timu pinzani ambayo hadi sasa hakuna mchezaji yeyote aliyeifikia ingawa Baleke anainyemelea na akipangwa kesho, ataifikia.

Chama alicheza dhidi ya Simba akiwa na Zesco United ya Zambia mwaka 2014 ambapo timu yake iliibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0.

Baadaye, Chama alisajiliwa Simba alikitumikia kikosi chao kwenye mechi za kilele cha tamasha hilo mwaka jana, 2020, 2019 na 2018.

Kama atapangwa kesho, Baleke ataifikia historia hiyo ya Chama kwani alikuwamo katika kikosi cha TP Mazembe ambacho kilialikwa kucheza na Simba mechi ya kilele cha tamasha hilo 2021 timu yake iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Chama pia ameweka rekodi nyingine ambayo nayo inaweza kufikiwa na Baleke ambayo ni ile ya kuwa mchezaji pekee aliyezifungia timu mbili tofauti bao katika mechi za kilele cha tamasha hilo.

2014, Chama alifunga bao moja katika ushindi wa mabao 3-0 ambao timu yake wakati huo ya Zesco iliupata dhidi ya Simba lakini mwaka 2020, akafunga bao moja wakati Simba ilipoibamiza Vital’o kwa mabao 6-0.

Baleke akifunga dhidi ya Dynamos, ataifikia rekodi hiyo ya Chama kwani tayari alishaifunga Simba wakati ilipopoteza dhidi ya TP Mazembe kwa bao 1-0. Soma zaidi kuhusiana na Simba Day kuanzia ukurasa wa saba ndani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: