Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama, Phiri wabebeshwa mabomu kuiua Vipers

Phiripic Chama, Phiri wabebeshwa mabomu kuiua Vipers

Tue, 7 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba, Mbrazil, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amewapa kazi maalum viungo wake washambuliaji, Clatous Chama na Moses Phiri wote raia wa Zambia kutibua mipango ya wapinzani wao Vipers.

Hiyo ni katika kuelekea mchezo wa marudiano wa Kundi C kunako Ligi ya Mabingwa Afrika, utakaopigwa leo Jumanne kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Timu hizo katika mchezo uliopita uliochezwa kwenye Uwanja wa St Mary’s, Uganda, Simba ikiwa ugenini ilishinda kwa bao 0-1, mfungaji akiwa Mkongomani, Hennock Inonga.

Akizungumza nasi, Robertinho alisema ameshamaliza mazoezi ya kimbinu na kiufundi yatakayowapa ushindi katika mchezo huo ambao ni muhimu kuchukua pointi tatu.

“Katika mchezo wa awali tuliocheza Uganda dhidi ya Vipers, Kibu (Denis), Saido (Saidi Ntibazonkiza) niliwapa kazi ya kuwavuruga mabeki wao kwa kutokuwepo mchezaji maalum wa kusimama katikati yao.

“Hiyo iliwafanya mabeki wa Vipers kutojua mchezaji yupi wa kumkaba, ilituwezesha kupata ushindi ugenini, hivyo ninataka kuona tukiingia na mbinu nyingine za ushindi kesho (leo).

“Ninataka kuwaona Chama na Phiri wakitimiza majukumu ambayo nimewapa mazoezini kwenda kufanyia kazi katika mchezo huo ambayo ni kufunga na kutengeneza nafasi za kufunga,” alisema Robertinho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: