Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama, Kibu wana kadi, akili yetu sasa kombe la shirikisho - Ahmed

Simba Horoya Sd.jpeg Chama, Kibu wana kadi, akili yetu sasa kombe la shirikisho - Ahmed

Thu, 4 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahemd Ally amesema kwa walipofikia mpaka sasa kikosi hicho hakina matumanini tena ya kubeba ubingwa wa Logi Kuu Tanzania Bara kwani wamepoteza mechi wao wenyewe na kujiweka katika mazingira magumu ya kuwafukuzia wapinzani wao, Yanga Sc wanaoongoza Ligi.

Ahmed amesema hayo jana Jumatano, Mei 3, 2023 wakati akizungumza na wanahabari mara baada ya mchezo wao dhidi ya Namungo ambapo Simba aliambulia sare ya bao 1-1 katika Dimba la Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.

“Mechi imekuwa nzuri na ngumu, tulitegemea upinzani kama huu, Namungo ni timu nzuri na gumu na leo wameonyesha kwa vitendo, tumepata alama moja tunamshukuru Mungu, tugaganga yajayo.

“Wachezaji wengi wana kadi za njano kwa hiyo tusingeweza kuwatumia, pia tuna mchezo mwingine jumapili wa nusu fainali ya ASFC dhidi ya Azam FC, kwa hiyo imelazimika kuwapumzisha ili kuwapa nafasi kwenye mchezo ujao.

“Chama ana kadi mbili za njano, Kibu Denis, Kapombe, Tshabalala wote wana kadi mbili za njano, kwa hiyo ilikuwa ni hatari kuwachezesha sababu endapo wangepata kadi nyingine ya njano maana yake anauoksa mchezo unaofuata dhidi ya Azam.

“Haya yalikuwa mabadiliko ya lazima ya mwalimu ili kuwanusuru wachezaji wasipate kadi ya tatu ya njano wasikose mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho. Ni tofauti na kusema mwalimu ameamua tu kuwapumzisha, mechi zote zilizosalia kwetu ni muhimu.

“Mechi ya Azam ni ya kuhimu sana kwetu, mashindano yote matatu tumeondolewa lakini akili yetu imehamia kwenye Kombe la Shirikisho.

“Waliocheza wameonyesha uwezo wao lakini ni wachezaji wa Simba wanapaswa waonyeshe kuipambania nemboi ya simba, ubora wa namungo umewadhibiti. Tuendelee na mapambano kila mtu ashike upande wake.

“Kwa hapa tulipofika kila mtu anaweza kuchagua upande wake, wa kukata tamaa, ana haki ya kukata tamaa wa kupambana tuendelee kupambana lakini tumejiweka kwenye hali mbaya na mambo ni magumu kweli,” amesema Ahmed Ally.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wao kinara, Jean Baleke dakika ya 27, kabla ya Salum Kabunda kusawadhisha dakika ya 39 kufuatia mpira wa kona aliouokoa kipa wa Simba Ally Salum ukadondoka kwenye miguu ya Kabunda.

Simba wanaendelea kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara wakiwa na alama 64 na michezo 27 nyuma ya Yanga wenye alama 68 na michezo 26.

Kwa matokeo hayo ya Simba, Yanga ambao kesho wataingia dimbani kukipiga na Singida BS kwenye Dimba la Liti, wanahitaji kushinda michezo miwili tu ili watangaze ubingwa wa ligi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: