Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CSKA Moscow watua Yanga kwa kazi maalum

Yanga Maafisaaaa CSKA Moscow watua Yanga kwa kazi maalum

Fri, 21 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imepokea ugeni wa Maafisa wa klabu ya CSKA Moscow ya Urusi ambao wamekuja kuendesha programu maalumu ya kutambua vipaji vya wanasoka chipukizi nchini.

Programu hii itaendeshwa na CSKA Moscow kwa kushirikiana na Young Africans Sports Club, itaanza leo Juni 21 na itafanyika Dar Es Salaam, Tanga na Zanzibar.

Baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Maafisa hao walikutana na uongozi wa Yanga chini ya Rais, Hersi Ally Said.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: