Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CEO Yanga atua Cairo, kushuhudia droo ya robo fainali CAF

Qndre Yanga Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Yanga, Andre Mtine

Tue, 4 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imemtuma tena Ofisa Mtendaji wao Mkuu Andre Mtine kufuatilia droo ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika sambamba na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mtine ameondoka nchini leo jioni tayari kwa hafla hiyo itakayofanyika kesho jijini Cairo kuanzia saa 3:30 usiku ambapo Yanga ni moja kati ya 8 zitakazosubiri kujua watakutana na timu ipi kwenye hatua hiyo kwa upande wa shirikisho.

Hii ni mara ya pili kwa Mtine kuhudhuria hafla hiyo ambapo awali alikuwa katika hafla kama hiyo wakati wa kupangwa makundi ya mashindano hayo.

Yanga imefuzu hatua ya robo fainali baada ya kuongoza kundi lao D wakimaliza vinara wa kundi hilo ikiwa ni mara ya kwanza kuongoza makundi katika historia ya klabu hiyo na kesho itaingia mazoezini kuanza maandalizi ya mechi ijayo dhidi ya Geita Gold.

Timu tatu ambazo moja inaweza kungukia kwa Yanga ni USM Alger (Algeria), Pyramids (Misri) na Rivers United (Nigeria) huku Yanga akitarajiwa kuanzia ugenini na kumalizia nyumbani kufuatia kuongoza kundi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: