Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#Breaking: Kipa Mbrazil atambulishwa Simba

Jefferson Brazil Jefferson Luis Szerban de Oliveira.

Sun, 23 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba imevuka ya Bara la Afrika mpaka bara la Amerika ya Kusini kumchukua nyanda Jefferson Luis Szerban de Oliveira (29) raia wa Brazil, ambaye atalinda lango lao msimu huu kwa mkataba wa miaka miwili.

Kupitia taarifa ya Klabu ya Simba imebainisha kuwa imemsajili Luis, akitokea katika Klabu ya Resende FC ya Brazil ambapo msimu aliichezea Itabrito FC-MG kwa mkopo.

Jefferson alikuwa akitajwa kujiunga na Simba kwa muda mrefu kuchukua mikoba ya Beno Kakolanya ambaye ameshaondoka klabuni hapo huku kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula akiendelea kurejea mazoezini polepole baada ya kufanyiwa upasuaji.

Vipi unauonaje usajili huu?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: