Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#Breaking: Inonga apewa 'Thank You' na Simba

Dzc Inonga Far Henock Inonga.

Mon, 24 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu Simba imefikia makubaliano ya kumuuza mlinzi wa kati, Henock Inonga kwenda FA Rabat inayoshiriki Ligi Kuu nchini Morocco.

Inonga raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amebakisha Mkataba wa mwaka mmoja unaomalizika 2025 lakini kutokana na klabu kujali na maslahi ya wachezaji, imemruhusu beki huyo kuondoka kwenda kujiunga na FA Rabat.

Simba imevuna dola 200,000 ikiwa ni sawa milioni 525 kwa kumuuza mlinzi Henock Inonga kwenda FAR Rabat

Inonga alijiunga na kikosi Cha Simba mwaka 2021 akitokea DC Motema Pembe ya Congo.

Katika kipindi cha miaka mitatu alichodumu ndani ya kikosi Cha Simba Inonga amekuwa muhimili wa timu na makocha wote waliopita wamekuwa wakimpa nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Mwaka 2022 Inonga alichaguliwa mlinzi bora wa Ligi kuu ya Tanzania baada ya kuonesha kiwango bora katika msimu huo.SIMBA Yamuuza Henock Inonga

Uongozi wa Simba umemshukuru Inonga kwa utumishi wake ullotukuka katika kipindi chote alichokuwa Simba na pia imemtakia kheri katika maisha yake mapya ya soka nje ya Simba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: