Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bosi Geita amkataa Mayele

Mayele Hat  Trick Bosi Geita amkataa Mayele

Tue, 21 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari wa Geita Gold, Hemed Kivuyo, amefunguka kuwa, hatishwi na wachezaji wa Yanga hasa Fiston Mayele ambaye hana kiwango bora zaidi ya wachezaji wao.

Ikumbukwe kwamba, Geita Gold watakuwa na kibarua cha kusaka alama tatu mbele ya Yanga katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) ambapo mechi hiyo inatarajiwa kupigwa kati ya Machi 30 na Aprili 2, mwaka huu.

Akizungumza nasi, Kivuyo alifunguka kwamba: “Droo nimeiona, tunafahamu kuwa Yanga ndiye bingwa mtetezi wa michuano hii, lakini kilichobaki kwa upande wetu ni kusubiri siku husika na kuingia uwanjani kuzisaka alama tatu.

“Yanga ni timu ya kawaida ila tunawaheshimu kwa sababu ni timu yenye umri mrefu kuliko sisi na wana mashabiki wengi zaidi, lakini ukiachana na hayo hakuna chochote ambacho wanatuzidi.

“Ubora wa wachezaji wao hauna utofauti na wachezaji wetu, huwezi kumfananisha Fiston Mayele na Daniel Lyanga, huwezi kumfananisha Kelvin Yondani na Bakari mwamnyeto, hizo ni ngazi mbili tofauti.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: