Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bocco awaomba radhi mashabiki wa Simba

Bocco Pic Bocco awaomba radhi mashabiki wa Simba

Thu, 4 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha wa Simba, John Bocco amewaomba msamaha mashabiki wa klabu hiyo kufuatia matokeo ya sare ya bao 1-1 waliyoyapata jana usiku katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Namungo FC mchezo uliofanyika Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.

Akizungumza na HabariLEO, nahodha huyo amekiri kuwa matokeo hayo yamefifisha matumaini yao ya kufukuzia ubingwa hasa kama wapinzani wao Yanga watashinda mchezo wa leo dhidi ya Singida Big Stars.

“Ni matokeo ambayo hata sisi wachezaji hatukuyategemea na yametumiiza pia, ndio maana kwa niaba ya wachezaji wenzangu tunaomba msamaha tutahakikisha tunapambana ili kushinda mechi tatu zilizobakia na kupigania ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), ili kuwapa furaha mashabiki wetu,” amesema Bocco.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: