Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bocco akiri mziki wa Yanga ni hatari

John Bocco Simba Sfsd John Bocco.

Mon, 14 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha wa Klabu ya Simba, John Bocco amewapongeza wapinzani wao Yanga Sc katika mchezo wa jana wa Fainali ya Ngao ya Jamii ulipigwa katika Dimba la CCM Mkwakwani Tanga.

Mchezo huo ulimalizika dakika 90 kwa timu zote kutoka sare ya bila kufungana hivyo wakalazimika kwenda kwenye changamoto ya mikwaju ya penati ambapo Simba walifanikiwa kushinda kwa kufunga penati 3-1.

"Tunamshukuru Mungu kupata kikombe baada ya miaka (2), mpinzani wetu (Yanga) amecheza vizuri kuanzia kipindi cha kwanza na kipindi cha pili pia niwapongeze.

"Tulikuwa tumesimama katika mpango wa mwalimu, tumepambana kwa ajili ya timu yetu na tunamshukuru Mungu kwa kutimiza ndoto hii.

"Ally Salim ameonyesha kuwa amekuwa na amekomaa, mchezo ha hatu tuliyokuwa ni ngumu lakini ameonyesha anaendelea kukua vizuri, tunampongeza na tunamwambia aendelee kujifunza, tunaamini atafika mbali sana," amesema John Bocco.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: