Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barbara afunguka alivyoteseka kumsajili Adebayo

Barbara Na Adebayor Barbara afunguka alivyoteseka kumsajili Adebayo

Mon, 20 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez amethibitisha kwamba alikuwa anafanya kila namna ili kupata saini ya Victorean Adebayo raia wa Niger kwenye kikosi cha Simba.

Akizungumza na mwandishi wa habari maarufu Afrika kutoka nchini Ghana, Micky Jr na kuongeza kuwa kipingamizi alikuwa ni mmoja wa viongozi wa soka la Niger baada ya kukataa ofa ambayo waliipeleka Simba.

"Siku tatu zilizopita nilikuwa na mazungumzo na aliyekuwa CEO wa Simba SC ambaye alithibitisha kuwa kila kitu kilikuwa tayari kwa ajiri ya kumsajili Victorien Adebayor lakini Rais wa Shirikisho la Soka la Niger aligoma biashara hiyo isifanyike na kumuuza RS Berkane," amesema Micky.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: